Riadha: Joshua Cheptegei avunja rekodi ya dunia ya mbio za kilomita 10 Valencia

Joshua Cheptegei amevunja rekodi ya duniani katika mbio za kilomita 10 huko Valencia, na kuweka rekodi mpya ya dakika 26 na sekunde 38.

Raia huyo wa Uganda mwenye umri wa miaka 23 amevunja rekodi iliyowekwa na mkenya Leonard Komon mwaka 2010 kwa sekunde sita.

Mganda huyo alizawadiwa kitita cha milioni 10,000 mwezi Oktoba huko Doha, baada ya kushinda mashindano ya mbio kimataifa ya 10km zilizofanyika Denmark mwezi Machi.

Mwaka 2018, aliweza kukimbia kwa dakika 41 na sekunde tano huko Nijmegen, Netherlands na kuvunja rekodi ya dunia katika mbio za kilomita 15.

Wastani wa mbio za Cheptegei ilikuwa dakika mbili na sekunde 40 kwa kilomita Valencia na 5km alitumia dakika 13 na sekunde 24.

“Huu mwaka ni mzuri kwangu” aliongeza. “Siamini kilichonitokea.

“Nilijua kuwa mashindano ya Valencia yatakuwa magumu na haraka zaidi duniani.Hivyo mimi kutunukiwa ushindi huu ni mafanikio makubwa sana.”

CHANZO: BBC SWAHILI

Leave a Reply

Close Menu